Usiku wa kuamkia leo ndani ya kanisa la kisasa nchini la City Christian
Centre (CCC) Upanga jijini Dar es salaam kumefanyika tamasha la usiku wa
kuabudu (Night of Worship) ambao ulikuwa wa aina yake na kubariki wengi
waliohudhuria ambapo Mungu alijichukulia utukufu baada ya watu zaidi ya
10 kumpa Yesu maisha yao pamoja na kufanyika maombi ya kuwafungua watu
kutoka katika vifungo mbalimbali yaliyoongozwa na askofu mkuu wa pili
mstaafu wa T.A.G Renwall Mwanisongole ambaye ndiye mchungaji kiongozi wa
kanisa hilo.
Vikundi vilivyoongoza watu katika kumsifu Mungu ni pamoja na The Next level, Neema Gospel Choir (N.G.C) kutoka AIC Chang'ombe ambao uimbaji wao umebadilika sana kutokea upigaji hadi uimbaji kwa ujumla na kubariki wengi waliohudhuria kanisani hapo, pia kulikuwa na vikundi vingine vingi ambavyo vilifanyika baraka kwa mamia ya waliofika katika usiku huo wa kuabudu.